Thursday, March 29, 2012

HUYU NDIO BINTI MBRAZIL MWENYE NYWELE NDEFU, ANAZIUZA!

 
.
Mrembo wa Kibrazil mwenye umri wa miaka 12 Natasha Moraes de Andrare ameamplfy kwamba ameamua kuziuza kwa pound 3,500 nywele zake ndefu ambazo zinamlazimu kuzishika anapotembea, akitarajia kwamba pesa hiyo itayaboresha maisha yake.
Ukubwa wa nywele zake unamnyima uhuru wa kufanya mambo mengi, akitoka tu shuleni ni nyumbani, hawezi kuogelea pamoja na kushiriki kwenye mambo mengine mengi kwa sababu nywele hazimpi uhuru, mpaka walimu wamemshauri azikate hizo nywele ambazo hajawahi kuzikata toka azaliwe.
Pamoja na ukubwa wa nywele zake bado rekodi ya kitabu cha Guinness cha rekodi za dunia, nafasi ya mtu mwenye nywele ndefu inashikiliwa na mchina Xie Qiuping ambae urefu wa nywele zake ni 5.63 metres.
(stori kutoka http://www.jestina-george.com/)
.
.
.

No comments:

Post a Comment