Tuesday, April 10, 2012

THIS IS IT!!! GONE BUT NEVER WILL U BE FORGOTTEN, REST IN PEACE STEVEN KANUMBA...!!!

 Baadhi yaa Waombolezaji wa msiba wa Steven Charles Kanumba wakiwasili kwenye Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam mchana huu kwa tendo la kuuhifadhi mwili wa Marehemu katika nyumba yake ya Milele

 Eneo litakalowekwa jeneza lenye mwili wa Marehemu Steven Kanumba kwa ajili ya kuzikwa kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,mchana huu.
 Mwili ukiwasili kwenye Makaburi ya Kinondoni

 Jeneza Lenye  Mwili wa Marehemu Steven Charles Kanumba ukiingizwa kaburini
Mama Mzazi wa Marehemu Steven Charles Kanumba akiwasili Makaburini huku akiwa ameambatana na Dada Asha Baraka.
 Mama mzazi wa Steven Charles Kanumba akiaga mwili wa mwanae makaburini Kinondoni baada ya zoezi hili kushindikana pale Leaders Club kutokana na msongamano kuwa mkubwa kupita kiasi. 
"Kwaheri mwanagu na upumzika kwa amani"
Ee Mungu msaidie huyu mama na umtie nguvu
Waombolezaji wakiwa wameshika mashada ya maua
 Kaburi la marehemu Kanumba likisakafiwa
 Dah kweli Kanumba umesimika kama mshumaa1 R.I.P we will miss you
Model Millen Magese akiwa na mashada ya maua

LIVE KUTOKA KINONDONI MAKABURINI KWENYE MAZISHI YA STEVEN KANUMBA

Hii ni barabara ya Kinondoni kuingia kwenye makaburi ya Kinondoni ilikuwa ni balaaaa yani dah, kule mbele ndio mwili wa marehemu Steven Kanumba ndio unakuja

 Kwa wingi wa watu ilibidi watu wapande juu ya miti lakini baadae waliamuriwa washuke chini na kamanda Kova

 Ray akiwa aamini kama swaiba wake ndio anakwenda kwenye nyumba yake ya milele

 Charlz Baba akiwa na wenzake kutoka Mashujaa Band, Charz ameniambia walikuwa wanatokea Morogoro so waliweza kuwahi makaburini

LIVE KUTOKA LEADERS CLUB KWENYE MAZISHI YA STEVEN KANUMBA

 Wanakwaya wakiimba nyimbo za uzuni.

Hii ndio sehemu ambayo mwili wa marehemu Kanumba unatarajiwa kuwekwa 

 Hawa watoto wanaopita ndio watoto waliokuwa wakicheza movie na marehemu Kanumba enzi ya uhai wake

 Mama yake Kanumba aliyenyoosha mkono juu kuwapungia watu waliokuja uwanjani

 Huyu dada hapa mbele alikuwa akilia kwa uchungu sana hadi nilikuwa namuonea huruma

 Hemed na Yusuph Mlela wakiingia

Makamu wa rais Dk. Mohamed Ghalib Bilali 

 Mke wa rais Mama Salma Kikwete

Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi akitoa heshima zake za mwisho kwenye mwili wa marehem.