Sunday, May 6, 2012

Diamond akishuka kwenye gari.
ICON katika mziki wa Bongofleva Naseeb Abdul ‘Diamond’ jana alitoa msaada katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre ambacho mwanamuziki TID anadaiwa kula fedha za yatima wanaoishi katika kituo hicho kilichopo Kinondoni Hananasif jijini Dar.
Akizungumza na mtandao huu kabla hajakabidhi msaada huo, Diamond alisema kuwa kikubwa zaidi kilichomfanya hadi atoe msaada huo ni kuguswa na maisha wanaoishi  yatima hao.
“Unajua siku zote Mungu anasema unachokipata ugawane na wenzako, sasa mimi pamoja na meneja wangu Joffrey a.k.a Joff tumeona tutoe nusu ya kile tulichokipata  kwa hawa ndugu zetu wanaolelewa katika kituo hiki,” alisema Diamond.…

Diamond akishuka kwenye gari.
ICON katika mziki wa Bongofleva Naseeb Abdul ‘Diamond’ jana alitoa msaada katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre ambacho mwanamuziki TID anadaiwa kula fedha za yatima wanaoishi katika kituo hicho kilichopo Kinondoni Hananasif jijini Dar.
Akizungumza na mtandao huu kabla hajakabidhi msaada huo, Diamond alisema kuwa kikubwa zaidi kilichomfanya hadi atoe msaada huo ni kuguswa na maisha wanaoishi  yatima hao.
“Unajua siku zote Mungu anasema unachokipata ugawane na wenzako, sasa mimi pamoja na meneja wangu Joffrey a.k.a Joff tumeona tutoe nusu ya kile tulichokipata  kwa hawa ndugu zetu wanaolelewa katika kituo hiki,” alisema Diamond.

Baadhi ya mizigo ambayo ilitolewa kama msaada katika kituo hicho ikiwa bado haijashushwa kwenye gari.
Diamond akishauriana kitu na meneja kitu wake Joff.
Diamond akiangalia mizigo jinsi inavyoshushwa.
Diamond akimsaidia mama yake kubeba mzigo.
Baadhi ya watoto wakiwa wamezunguruka misaada iliyotolewa na Diamond.
Diamond akiwa amempakata mmoja wa watoto yatima.
Baadhi ya misaada iliyotolewa.
Diamond na meneja wake Joff wakiwa wamewapakata watoto.
Diamond na Joff wakikabidhi misaada.
Diamond , mama yake pamoja na mmoja wa wasimamizi wa kituo hicho wakishuhudia Joff akikabidhi msaada.
Diamond akiwa amelala kwenye kitanda cha watoto yatima hao.
Mtangazaji wa Clouds Tv, Shedee akibadilishana mawazo na mtangazaji mwenzie kituo hapo.
Diamond akiangalia jinsi Joff anavyosaini kitabu cha wageni.
Diamond naye akisaini kitabu cha wageni.
Mmoja wa watoto yatima akisoma dua mara tu ya kukabidhiwa misaada.

Tuesday, May 1, 2012

 

This Blog
Linked From Here
MY BLOG LIST/TOVUTI ZINGINE
This Blog
 
 
 
 
Linked From Here
 
 
 
MY BLOG LIST/TOVUTI ZINGINE
 
 
 

TASWIRA ZA SAFARI YA DIAMOND KUELEKEA DAR LIVE, MBAGALA NA HELIKOPTA KWA AJILI YA SHOW YAKE YA KIHISTORIA...!!!

Huyu ndiye Diamond mwingine hakunaga, akielekea kupanda helikopta kwenda viwanja vya Dar Live kufanya makamuzi jana Jumapili, 29 April 2012
Diamond akiwa na rubani wake wakielekea kwenye helikopta
Hapa nimemkubali maana hakuna kitu muhimu kama kujikabidhi mikononi mwa Mungu kabala ya kufanya jambo lolote
Yes Sir, Salute
Mashabiki full kupagwa baada ya kusikia helikopta ikiwasili na star wao
Helikopta ikingia uwanjani hapo chezeaaa
Dar Live palikuwa hapatoshi
Ilikuuwa patashika kwa mashabiki wa Diamond, Bless them
Helikopta ikamshushua ka kuondoka zake
Diamond akimsalute rubani wake na Mwenyezi Mungu kwa kumfikisha salama
Ni showbiz kwa kwenda mbele, hapa akisalimiana na mashabiki wake
Diamond akishuka kwenye gari tayari kwenda kufanya makamuzi
 Nimpende nani? Nimpende nani? hahaha nawaza kwa sauti tu

 full mzuka
 Mambo ya mavazi ya Diamonda na dancers wake naona yalikuwa ni mwendo wa US Marine Style
 Diamond akiwa amebebwa na dancers wake
 makamuzi yakiendelea
 Alitishajee
 Dar Live palikuwa hapatoshi
 Wakali Dancers walisindikiza show ya Diaomond
 Pamoja na mvua kubwa kunyesha mashabiki waliendlea kuburudika
Bwana misosi akikamua usiku wa jana
 Timbulo nae alikuwepo kukoga mashabiki
 Timbulo akiendelea na makamuzi
 Msanii wa kundi la Pah One akikamua

 Mvua haikuzuia show kuendelea
Mashabiki wakifurahia show

Wednesday, April 25, 2012


Baada ya kuumiza watu vichwa kwa muda mrefu hatimaye hiki ndicho alichokiandika DIAMOND kwenye BlackBerry Messenger ambapo kwa idhini yake mwenyewe millardayo.com ilimwambia itaitumia.... 

Kulikua na stori kibao mtaani kwamba DIAMOND PLATNUMS yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi na mrembo JOKATE lakini bado ilikua haijathibitika, sasa hivi ndio kaamua kuweka wazi na habari ndo hiyooooooo. Tunawataki akila la heri wapendanao hawa.

Habari hii ni kwa hisani ya
 

Sunday, April 15, 2012

KWAMARA NYENGINE TENA DIAMOND AFUNIKA NA KUSHINDA TUZO TATU KWENYE KILI MUSIC AWARD 2012...!!!

 
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya (Bongofleva) Nassib Abdul a.k.a Diamond ameng’ara kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Award 2012, baada ya kujinyakulia tuzo tatu.“Namshukuru Mungu, wakati mwingine uvumilivu na subira ni mzuri. Mwaka jana sikupata tuzo, nikamshukuru Mungu, nikaongeza bidii, nikafanya kazi nzuri, leo nimeibuka  na tuzo tatu”,alisema.Tuzo hizo ni ( Mtunzi Bora wa nyimbo,tuzo ya video bora ya Mwaka –moyo wangu na tuzo ya Mtumbuizaji bora wa kiume.
 Mwanamuziki Diamond (kulia)akipokea tuzo yake kutoka kwa George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro mara baada ya kutangazwa mshindi wa utunzi bora wa nyimbo katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki bora  Kilimanjaro Music Award 2012 zinazofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na kuhudhuria na waalikwa mbalimbali pamoja na wadau wa muziki kutoka ndani ya Tanzania  na nje ya nchi.
Muigizaji/mchekeshaji Mahiri wa kikundi cha Vuvuzela Entertainment,Evans Bukuku akimkabidhi tuzo yake msanii Diamond,ya video bora ya mwaka.

Mkali wa hip hop Tanzania,Chid Benz akimkabidhi tuzo nyingine msanii Diamond ya mtumbuizaji bora wa kiume.
Mama yake Diamond na Professor Jay wakishangilia ushindi wa Diamond
---
Mwimbaji Nyota wa Bongo Fleva Nassib Abdul a.k.a Diamond usiku wa Aprili 14,2012 ameibuka kidedea baada ya kujinyakulia tuzo tatu katika tamasha la Utoaji Tuzo za Kili Music Award 2012.

Diamond ambaye mwaka 2010 aliibuka pia kidedea kwa kuzoa tuzo nyingi na mwaka 2011 kumpa nafasi 20% kwa kuzoa tuzo nyingi mwaka huu amenyakua tuzo ya MTUNZI BORA WA MWAKA, MTUMBWIZAJI BORA WA KIUME na Video yake ya Mawazo ikinyakua tuzo ya VIDEO BORA YA MWAKA.

Mbali na Diamond aliyebahatika kunyakua Tuzo mbili katika tuzo hizo ni msanii mwingine wa Bongo Fleva Suma Lee aliyenyakua tuzo za WIMBO BORA WA AFRO POP ambao alipata kupitia wimbo wa HAKUNAGA na Tuzo ya pili ni ya WIMBO BORA WA MWAKA.
Ambao pia ni HAKUNAGA.

Aidha msanii Chiopukizi wa Bongo Fleva, Omy Dimpoz nae ametamba baada ya kunyakua tuzo ya WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA wa  NAI NAI aliomshirikisha ALI KIBA na pia alitwaa tuzo ya MSANII BORA ANAECHIPUKIA kupitia wimbo wake huo huo wa NAI NAI.

Nae Roma Mkatoliki a.k.a Mpare wa milimani alikuwa katika kundi hilo la wasanii wenye tuzo mbili baada ya kupata tuzo ya WIMBO BORA WA HIP HOP wa  MATHEMATICS na Tuzo ya MSANII BORA WA HIP HOP.

Wasanii na Vikundi vingine ambavyo vilijinyakulia tuzo ni pamoja na  WIMBO BORA WA RAGGAE Ulikuwa ni ARUSHA GOLD wa kundi la WARRIORS FROM EAST huku Tuzo ya WIMBO BORA WA DANCE HALL ukiwa ni MANENO MANENO wa QUEEN DARLIN.

Tuzo ya WIMBO BORA WA ZOUK RHUMBA alienda kwa Ali Kiba kupitia wimbo wake maarufu wa DUSHELELE , Tuzo ya WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA KIASILI ilikwenda kwa A.T kwa kibao cha VIFUU UTUNDU.

Tunzo nyingine ilikuwa ni ya  WIMBO BORA WA TAARABU aliyonyakua mwana dada wa kikurya anaeimba Taarabu Aisha Mashauzi kupitia wimbo wa NANI KAMA MAMA wa kundi lake la Mashauzi Classic.

Kundi la Twanga Pepeta nalo lilijinyakulia Tuzo ya WIMBO BORA WA KISWAHILI kupitia wimbo wa DUNIA DARAJA huku Tuzo ya WIMBO BORA WA R&B.
Ikienda kwa Ben Paul kwa wimbo wa NUMBER ONE FAN.

Tuzo nyingine katika mfululizo huo wa Kili Music Award 2012 ilikwenda kwakalijo Kitokololo aliyepata Tuzo ya RAPA BORA WA BAND ambapo Tuzo ya WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI ilienda kwa Wimbo wa KIGEUGEU uliyoimbwa nae JAGUAR.

Tuzo zingine ni za MTUMBWIZAJI BORA WA KIKE iliyoenda kwa KHADIJA KOPA, tuzo ya  MTAYARISHAJI BORA WA MAPIGO YA MUZIKI ilienda kwa MANEKE.

Tuzo ya HALL OF FAME ilienda kwa TAASISI JKT, Tuzo ya HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI ilienda kwa Mtu mzima KING KIKII na HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI Ilinyakuliwa na Hayati REMMY ONGALA.

Mkonngwe wa uimbaji wa nyimbo za Kibongo Judith Wambura Habash “Lady Jay Dee alinyakua tuzo ya ya MWIMBAJI BORA WA KIKE huku kijana aliyeshika kasi kutoka kundi la THT Barnaba akifunga jahazi hilo kwa kunyakua tuzo ya MWIMBAJI BORA WA KIUME.